• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China ashiriki katika uzinduzi wa Jumba la Urafiki kati ya Vietnam na China

  (GMT+08:00) 2017-11-13 09:50:43

  Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini Vietnam amehudhuria sherehe ya uzinduzi wa Jumba la Urafiki kati ya Vietnam na China iliyofanyika jana huko Hanoi.

  Jumba hilo lenye eneo la mita za mraba 13,800 ni mradi muhimu uliofadhiliwa na China nchini Vietnam.

  Rais Xi alikaribishwa kwenye jumba hilo na mwenyekiti wa bunge la nchi hiyo Bi. Nguyen Thi Kim Ngan, na wawakilishi wa makampuni ya China na Vietnam.

  Rais Xi na Bi. Ngan pia walizindua kituo cha utamaduni wa China ndani ya jumba hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako