• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Taifa Stars yailazimisha sare Benin

  (GMT+08:00) 2017-11-13 10:06:21
  Tanzania imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Benin katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jana mjini Cotonou.

  Katika mchezo huo uliochezeshwa na waamuzi kutoka Benin, Ligali Praphiou aliyesaidiwa na Bello Razack na Koutou Narcisse, hadi mapumziko wenyeji The Squirrels, walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa kwa penalti na Nahodha, Stephane Sessegnon anayechezea klabu ya Montpellier ya Ufaransa.

  Goli la kusawazisha kwa Tanzania lilifungwa na mchezaji wa klabu ya Dhofar ya Oman, Elias Maguri aliyefunga bao hilo akimalizia krosi ya winga Shiza Kichuya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako