• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uswisi wafuzu kombe la dunia mwaka 2018

  (GMT+08:00) 2017-11-13 10:07:41
  Ndoto za timu ya taifa ya Ireland ya Kaskazini za kufuzu mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka 2018 zimezimika jana baada ya matokeo ya sare tasa kwenye mechi ya pili ya mtoano dhidi ya Uswisi iliyopigwa jana mjini Basel.

  Ireland ambayo haijashiriki mashindano ya kombe la dunia tangu ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 1986, imekosa tena safari kufuatia kipigo cha goli 1-0 ilipofungwa ikiwa nyumbani katika mechi ya kwanza ya mtoano dhidi ya Uswisi.

  Kwa ushindi huo, Uswisi inakuwa timu ya 27 kufuzu michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuanza June 14 mwaka kesho nchini Urusi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako