• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sebastian Vettel ashinda mbio za langalanga Brazil

  (GMT+08:00) 2017-11-13 10:09:37
  Licha ya kukabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa madereva wenzake, mjerumani Sebastian Vettel wa timu ya Ferari amefanikiwa kushinda mbio za langalanga za magari ya mwendokasi Brazil zilizofanyika jana mjini Sao Paulo.

  Katika mashindano hayo nyota mwingereza Lewis Hamilton wa Mercedes alifanikiwa kuongoza katika mizunguko kumi ya kwanza kabla ya kuadhibiwa alipokiuka moja ya kanuni za barabara ya mashindano jambo lililomfanya aishie nafasi ya nne, huku nafasi ya pili ikienda kwa Valtteri Botas wa timu ya Mercedes na Kimi Raikonnen wa Ferari akishika nafasi ya tatu.

  Huu ni ushindi wa tano kwa Vettel kwa mwaka huu pekee baada ya kushinda pia kwenye mbio za Australia, Bahrain, Ufaransa na Hungary.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako