• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Serikali ya Rwanda ina mpango wa kuanzisha mageuzi 15 mapya katika sekta mbalimbali za kufanya biashara

  (GMT+08:00) 2017-11-13 19:08:01

  Serikali ya Rwanda ina mpango wa kuanzisha mageuzi 15 mapya katika sekta mbalimbali katika miezi sita ijayo, kama njia ya moja ya kupunguza biashara katika nchi humu.

  Hatua hii imekuja baada ya ripoti ya biashara ya benki ya Dunia, iliyoweka Rwanda nafasi ya 41 kimataifa na nambari ya pili Afrika kati ya uchumi 190 duniani kote.

  Serikali ina mpango wa kuanzisha mageuzi tano mwezi Mei mwaka ujao, ili kuhakikisha usambazaji wa nishati ni wakutosha.

  Serikali pia inataka kupunguza muda wa kuunganishwa na umeme kutoka siku 34 sasa hadi siku 20.

  Mageuzi mengine ni pamoja na kuanzisha mpango wa huduma bora za umeme na kupunguza gharama ya kuunganishwa.

  Karim Tushabe, mkuu wa kitengo cha kufanya biashara katika Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), amesema marekebisho hayo yatahakikisha kuwa mipangilio ya umeme iliyopangwa haitaathiri uzalishaji wa wawekezaji.

  Akizungumza juu ya mageuzi yaliyopangwa, Mwenyekiti wa Shirikisho la Sekta Binafsi Benjamin Gasamagera amesema ikiwa mageuzi hayo yatatekelezwa, itasaidia kuboresha hali ya biashara nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako