• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonyesho ya viwanda ya China na Afrika yatoa jukwaa jipya la uwezo wa ushirikiano wa kiviwanda

  (GMT+08:00) 2017-11-13 20:53:19

  Maonyesho yatakayoanza hivi karibuni yatatoa jukwaa jipya kwa biashara ya China na Afrika katika kuimarisha ushirikiano wa uwezo wa kiviwanda.

  Makamu mwenyekiti wa Baraza la China la Kuboresha Biashara ya Kimataifa (CCPIT) Bw. Chen Zhou amesema, maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Baraza hilo yatakayofanyika kuanzia Desemba 13 hadi 16 jijini Nairobi nchini Kenya. Bw. Chen amesema, maandalizi ya maonyesho hayo ambayo yanafanyika Afrika kwa mara ya kwanza, yamekamilika.

  Kampuni 56 kutoka China zitashiriki kwenye maonyesho hayo ambapo zitaonyesha bidhaa za kiwango cha juu na teknolojia ya juu katika ujenzi wa reli na barabara, miundombinu, mawasiliano ya simu, mashine, uzalishaji, na mchakato wa uzalishaji wa bidhaa za mashambani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako