• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Saudi Arabia kufungua tena baadhi ya bandari na viwanja vya ndege nchini Yemen

  (GMT+08:00) 2017-11-14 08:48:07

  Jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia linatarajiwa kufungua tena bandari tatu na viwanja vitatu vya ndege vinavyodhibitiwa na serikali ya Yemen, lakini vile vinavyodhibitiwa na waasi vitaendelea kufungwa. Jeshi hilo lilifunga safari za barabara, anga na bahari kwenda Yemen baada ya Saudi Arabia kuzuia kombora lililorushwa na waasi wa Houthi dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh Novemba 4. Mkurugenzi wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa Bw. Mark Lowcock amesema wiki iliyopita kuwa Yemen inakabiliwa na njaa kubwa ambayo haikuwahi kutokea katika miongo iliyopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako