• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UN yatoa mwito wa kuondoa vizuizi ili kupitisha misaada ya kibinadamu kwa Yemen

  (GMT+08:00) 2017-11-14 09:07:26

  Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uratibu wa mambo ya kibinadamu OCHA, imesema athari ya vizuizi vilivyowekwa dhidi ya Yemen zimesababisha upungufu mkubwa wa bidhaa na vifaa vya misaada nchini humo.

  Watu wote nchini Yemen wanategemea uagizaji wa chakula, mafuta na dawa kupitia bandari. Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, zaidi ya milioni 17 wa Yemen hawawezi kupata chakula cha kutosha.

  Shirika la mpango wa chakula WFP limesema, zimebaki siku 111 kabla ya akiba ya mchele nchini Yemen kwisha, na siku 97 kabla ya akiba ya ngano kwisha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako