• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Israel yasema itaendelea na operesheni za kijeshi nchini Syria

  (GMT+08:00) 2017-11-14 09:07:51

  Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu, amesema ameziambia Marekani na Russia kuwa Israel itaendelea na operesheni za kijeshi nchini Syria.

  Bw. Netanyahu amesema, Israel inadhibiti mipaka yake, inalinda taifa lake, na itaendelea kufanya hivyo. Ameongeza kuwa Israel itaendelea na operesheni nchini Syria kutokana na mahitaji ya usalama wa Israel.

  Bw. Netanyahu alisema hayo siku mbili baada ya mkutano kati ya rais Donald Trump wa Marekani na rais Vladmir Putin wa Russia, ambapo wamekubaliana kupanua makubaliano ya usimamishaji wa mapambano yaliyofikiwa tarehe 7 mwezi Julai kwenye delta ya Kusini Magharibi kwenye mpaka wa Israel na Jordan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako