• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw Guterres asema Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia kukabiliana na tetemeko la ardhi lililotokea kwenye mpaka wa Iran na Iraq

  (GMT+08:00) 2017-11-14 09:54:47

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, umoja huo uko tayari kusaidia juhudi za kukabiliana na tetemeko kubwa la ardhi lililozikumba Iran na Iraq.

  Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric ametoa taarifa akisema, Bw. Guterres amesikitishwa na idadi kubwa ya vifo na majeruhi na hasara iliyotokana na tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.3 kwenye kipimo cha Richter lililotokea kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.

  Habari zinasema, watu zaidi ya 400 wamefariki na wengine elfu 7 wamejeruhiwa kwenye tetemeko hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako