• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yasisitiza kuwa itajitoa kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

  (GMT+08:00) 2017-11-14 10:03:17

  Marekani imetangaza tena kuwa itajitoa kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa itakapostahiki kufanya hivyo.

  Taarifa iliyotolewa na serikali ya Marekani imesema, msimamo wa Marekani wakati ilipojiunga na Mkataba wa Paris mwaka 2015, ambao unazitaka nchi karibu 200 kupunguza kwa hiari utoaji wa hewa ya ukaa inayosababisha kuongezeka kwa joto duniani, "haubadiliki".

  Taarifa pia inasema Marekani inataka kujitoa kwenye Mkataba wa Paris haraka iwezekanavyo, isipokuwa kama vifungu vya mkataba huo vitawanufaisha zaidi watu wa Marekani.

  Marekani imetangaza hayo wakati wa mazungumzo kuhusu hali ya hewa yaliyoanza Novemba 6 mjini Bonn, Ujerumani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako