• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China akutana na aliyekuwa rais wa Laos

  (GMT+08:00) 2017-11-14 10:06:07
  Rais Xi Jinping wa China jana alikutana na aliyekuwa katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha mapinduzi ya umma cha Laos na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Bw. Choummaly Sayyasone.

  Wakati wa mazungumzo yao, rais Xi Jinping ameeleza kuwa matokeo muhimu yaliyopatikana katika Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China yanasaidia kujenga uhusiano mpya wa kimataifa, na jumuiya yenye mustakabali wa pamoja yenye umuhimu wa kimkakati kati ya China na Laos, na kwamba lengo la ziara yake nchini Laos ni kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili ufikie kwenye ngazi mpya.

  Kwa upande wake Bw. Choummaly amesema Laos siku zote inafanya juhudi za kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya vyama na serikali za nchi hizo mbili, na kujitahidi kukuza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya pande mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako