• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwanamichezo Bora wa Afrika Kusini mwaka 2017

  (GMT+08:00) 2017-11-14 10:19:39
  Kamati ya olimpiki na Umoja wa Vyama vya michezo, nchini Afrika Kusini imemtangaza Nyota wa michezo ya kuruka Luvo Manyonga kuwa mwanamichezo bora wa taifa hilo kwa mwaka 2017, katika hafla ya utaoji za michezo iliyofanyika jijini Johannesburg.

  Manyonga ambaye ni mshindi wa medali ya fedha katika mchezo wa kuruka umbali mrefu kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 mjini Rio De Janeiro, alifanikiwa pia kuweka rekodi ya pekee barani Afrika mwaka huu kwa kuruka umali wa mita 8.65 na akifanikiwa kunyakua mataji mengi ndani na nje ya afrika Kusini.

  Kwa upande wake mwanariadha Caster Semenya alifanikiwa kujinyakulia tuzo ya mwanamichezo bora kwa upande wa wanawake nchini na Dyan Buis akitangazwa kuwa mwanamichezo bora kwa wachezaji wenye ulemavu nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako