• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNHCR kutafuta ufumbuzi wa msukosuko wa wakimbizi wa Waafrika

  (GMT+08:00) 2017-11-14 10:21:46

  Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema litaanzisha kampeni kabambe ya kutoa wito kwa Waafrika kuchukua hatua ya kutafuta ufumbuzi wa msukosuko wa wakimbizi barani humo.

  UNHCR imesema kampeni hiyo ijulikanayo kama "LuQuLuQu" inalenga falsafa ya Afrika ya "Ubuntu" au "Ujamaa" inayohimiza misingi na thamani ya wajibu wa pamoja, kutumia raslimali kwa pamoja, na kusaidiana, iliyorithi imani na utamaduni wa Afrika. Kampeni hiyo itakayozinduliwa Nairobi siku ya Jumamosi inawataka mamilioni ya watu barani ya Afrika, au wanaohusiana na Afrika, kuwakubali wakimbizi na na tatizo la kupoteza makazi kupita kujitolea kwa kuchukua hatua, kuhamasisha kujitegemea, ilio kuwapa uwezo wakimbizi.

  Kampeni hiyo itazinduliwa kwa pamoja kwenye nchi sita zikiwemo Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Ivory Coast na Senegal kwa mwezi huu mzima wa Novemba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako