• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Afrika yatakiwa kupunguza ushuru wa usafiri wa anga

    (GMT+08:00) 2017-11-14 19:06:55

    Waziri mkuu wa Rwanda Edouard Ngirente amesisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo inajitolea kuendelea kuunga mkono sekta ya usafiri wa anga.

    Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano wa 49 wa kila mwaka wa chama cha mashirika ya ndege barani Afrika Ngirente amesema Rwanda inaweka sera za kupunguza gharama za usafiri wa anga na pia kuondoa vikwazo.

    Alisema pia Rwanda imeanzisha mpango wa kutoa visa kwa wasafiri pindi tu wanapofika nchini humo ili kuwaondolea usumbufu wa kwenda kwenye ubalozi.

    Washiriki kwenye mkutano huo wa Kigali pia wametoa wito kwa serikali za Afrika kuboresha miundo mbinu ya usafiri wa angani na kupunguza ushuru husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako