• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Somalia yaahidi kuzidisha operesheni za kijeshi dhidi ya magaidi

  (GMT+08:00) 2017-11-14 19:27:58

  Somalia imeahidi kuzidisha operesheni za kijeshi dhidi ya wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS) na Al Shabaab ili kuleta utulivu nchini humo.

  Waziri wa habari wa nchi hiyo Abdurahman Omar Osman amesema, serikali itatumia rasilimali zinazopatikana, ikiwemo majeshi ya kigeni kutoka wenzi wa kimataifa ili kuwaondoa magaidi nchini Somalia. Amesema serikali itaendelea na operesheni za kijeshi, ikiwemo mashambulizi ya anga, dhidi ya kundi la Al Shabaab ili kujibu mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo dhidi ya raia, vikosi vya usalama vya Somalia, na Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM.

  Taarifa ya waziri huyo imekuja baada ya mfululizo wa mashambulizi ya anga yaliyoongozwa na jeshi la Marekani nchini Somalia, ambapo wapiganaji kadhaa wa kundi la IS na Al Shabaab waliuawa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako