• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirikisho la makampuni ya ndege ya Afrika latoa wito kuboresha usimamizi wa ndege barani humo

  (GMT+08:00) 2017-11-14 19:40:56

  Katibu mkuu wa shirikisho la makampuni ya ndege ya Afrika Bw. Elijah Chingosho ametoa wito wa kuboresha usimamizi wa ndege barani Afrika ili kusukuma mbele maendeleo ya usafiri wa anga katika bara hilo.

  Bw. Chingosho amesema, hivi sasa sekta ya usafiri wa anga barani Afrika inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa sera kamili ya usimamizi na usimamizi dhaifu wa usalama, ambayo yanazuia maendeleo ya sekta hiyo, na kuzihimiza serikali za nchi za Afrika kuchagua mfumo unaofaa zaidi wa usimamizi.

  Aidha, katibu mkuu wa kamati ya ndege za abiria ya Afrika Iyabo Sosina amesema, hivi sasa, kiwango cha utekelezaji wa kanuni ya safari za ndege za abiria la kimataifa hakijafikia asilimia 60. Nchi za Afrika zinapaswa kushirikiana na makampuni ya ndege kuboresha njia ya usimamizi ili kuhakikisha makampuni hayo yanafikia kanuni ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako