• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atuma salamu za rambirambi kwa Iran na Iraq kutokana na vifo vilivyosababishwa na tetemeko la ardhi

  (GMT+08:00) 2017-11-14 20:27:20

  Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za rambirambi kwa marais wa Iran na Iraq kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea jumapili karibu na mpaka wa nchi hizo mbili.

  Katika salamu hizo, rais Xi ameahidi kuziunga mkono nchi hizo mbili katika wakati huu mgumu, na kueleza kushtushwa na tetemeko hilo kubwa lililosababisha vifo vya watu 445 huku wengine zaidi ya elfu 7 wakijeruhiwa, huku wengine wakiwa bado wamefukiwa na vifusi.

  Pia rais Xi ameeleza imani yake kuwa watu wa Iran na Iraq, chini ya uongozi wa marais wao na serikali zao, watakabiliana na maafa haya na kujenga upya nchi zao.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, China iko tayari kutoa msaada unaohitajiwa na nchi hizo ili kusaidia wahanga wa tetemeko hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako