• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China asisitiza kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano katika Asia Mashariki

  (GMT+08:00) 2017-11-15 09:46:58

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amehudhuria mkutano wa 12 wa kilele wa Asia Mashariki nchini Philippines. Viongozi wa nchi 10 za Jumuiya ya nchi za Asia Mashariki ASEAN, rais Moon Jae-in wa Korea Kusini, waziri mkuu wa Russia Bw. Dmitry Medvedev, waziri mkuu wa Japan Bw. Abe Shinzo na mawaziri wengine kutoka nchi mbalimbali wamehudhuria mkutano huo.

  Akihutubia mkutano huo Bw. Li Keqiang amesema mkutano huo umekuwa unasukuma mbele maendeleo na kulinda usalama na utulivu wa kikanda, na kuwa jukwaa muhimu la mawasiliano na ushirikiano kwa nchi za kikanda na nchi kutoka kanda nyingine. Ametoa mapendekezo kadhaa ya kuimarisha ushirikiano katika eneo la Asia Mashariki, ikiwemo kuharakisha mafungamano ya kikanda, kuhimiza maendeleo ya jamii, na kukamilisha utaratibu wa usalama wa kikanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako