• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi za Afrika Mashariki zatoa mwito wa kudumisha amani kwenye majimbo yanayopambana ya Somalia

  (GMT+08:00) 2017-11-15 09:21:22

  Jumuiya ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD imetoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kudumisha na kujenga amani kati ya majimbo yanayopambana ya Puntland na Galmudug nchini Somalia.

  Taarifa iliyotolewa na IGAD baada ya mkutano wa siku mbili, inasema jumuiya hiyo itashirikiana na serikali kuu ya Somalia na serikali za majimbo ya Puntland na Galmudug, kutafuta suluhu ya kudumu ya mapambano ya udhibiti wa mji wa Galkayo.

  Kwa sasa mji wa Galkayo umegawanywa katika sehemu mbili, sehemu ya kusini inatawaliwa na serikali ya jimbo la Galmudug, na sehemu ya kaskazini inatawaliwa na serikali ya jimbo la Puntland.

  Mwezi Oktoba mwaka jana serikali za majimbo hayo mawili zilisaini makubaliano ya amani, na kukomesha mapambano yaliyosababisha vifo vya watu 50 na wengine elfu 90 kukimbia makazi yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako