• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Libya yakataa uamuzi wa bunge la mashariki wa kuwachunguza mameya

  (GMT+08:00) 2017-11-15 09:25:24

  Serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imekataa uamuzi uliotolewa hivi karibuni na bunge la mashariki, wa kuwasimamisha na kuwachunguza mameya wa miji mikubwa na midogo ya mashariki wenye uhusiano na serikali.

  Kwenye taarifa yake serikali imesema imehuzunishwa na vitendo vya kutowajibika vinavyozuia juhudi za serikali za kuondoa taabu za watu. Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa imesisitiza kuwa inapinga uamuzi huo unaozuia makubaliano, kuzidi kuwagawa watu, na kukiuka haki za msingi za raia.

  Waziri mkuu wa mpito wa mashariki Bw Abdullah Thanni, Jumapili alitoa amri ya kuwachunguza mameya wa miji mikubwa na midogo ya mashariki wenye uhusiano na serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako