• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wataalamu wa Afrika wajadili kuratibu udhibiti wa ndege zisizo na rubani

  (GMT+08:00) 2017-11-15 10:02:15

  Wataalamu wa usafiri wa anga wamekutana mjini Kigali, Rwanda kujadili uratibu wa usimamizi wa ndege zisizo na rubani.

  Wataalamu hao wameshiriki kwenye kongamano la siku tatu kuhusu mifumo ya kuendesha ndege zisizo na rubani, lililoandaliwa na Ofisi ya mashariki na kusini mwa Afrika katika Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga ICAO.

  Kongamono hilo limewashirikisha wataalamu 60 kwenye sekta za usafiri wa anga kutoka nchi 14 za mashariki na kusini mwa Afrika. Wataalamu hao watajadili changamoto za usafiri wa ndege zisizo na rubani ili kuepusha ajali.

  Kwenye kongamano hilo, waziri wa usafiri wa Rwanda Bw Jean de Dieu Uwihanganye amesisitiza umuhimu wa kuratibu usimamizi wa ndege zisizo na rubani, ili kuhakikisha zinatumiwa kwa njia halali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako