• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa fedha wa Tanzania asema deni la taifa bado linadhibitika

  (GMT+08:00) 2017-11-15 10:11:26

  Serikali ya Tanzania imesema deni la taifa, ambalo ni sawa na asilimia 31.2 ya jumla ya pato la taifa, bado linadhibitika.

  Waziri wa fedha wa Tanzania, Bw. Philip Mpango ameliambia bunge mjini Dodoma kuwa uwezo wa Tanzania wa kukopa unaweza kufikia asilimia 56 ya Pato la Taifa.

  Amesema hayo baada ya baadhi ya wabunge kulalamika kuhusu kuongezeka kwa haraka kwa deni la taifa.

  Bw Mpango amesema deni la taifa limeongezeka kwa dola za kimarekani bilioni 22.3 za mwaka 2016 hadi dola bilioni 26 za mwezi Juni, 2017.

  Ameongeza kuwa serikali itaendelea kukopa ili kufadhili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako