• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KPA Kikapu wanawake washinda mechi dhidi ya DCMP ya DRC

    (GMT+08:00) 2017-11-15 10:13:31
    Timu ya kikapu ya mamlaka ya bandari nchini Kenya jana imepata ushindi wake wa kwanza katika mashindano ya klabu bingwa Afrika Wanawake yanayoendelea nchini Angola baada ya kuifunga DCMP ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa vikapu 70-51.

    Ili kufuzu hatua ya mtoano KPA watalazimika kushinda mechi ya mwisho ya hatua ya makundi kesho dhidi ya Ferroviario De Maputo ya Msumbiji.

    Katika mechi nyingine ya kundi B iliyochezwa jana mabingwa watetezi wa michuano hiyo Primero De Agosto ya Angola wameilaza Ferroviario De Maputo ya Msumbiji kwa pointi 74-65.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako