• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamilioni ya watu wakabiliwa na hatari nchini Yemen kutokana na kufungwa kwa mpaka kwa wiki mbili

    (GMT+08:00) 2017-11-15 10:17:07

    Ofisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kibinadamu nchini Yemen ameonya kuwa mamilioni ya watu nchini humo wanakabiliwa na hatari kutokana na kufungwa kwa mipaka ya ardhi, bahari na anga.

    Mratibu wa mambo ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Bw. Jamie McGoldrick, amesema kuna watu milioni 21 nchini humo wanaohitaji misaada, na milioni saba kati yao wanakabiliwa na njaa na kutegemea msaada wa chakula.

    Amesisitiza kuwa mapambano nchini Yemen yaliyoanza mwezi Machi mwaka 2015, yamesababisha msukosuko mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani.

    Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pia limetahadharisha kuhusu hali ya kibinadamu inayozidi kuwa mbaya nchini Yemen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako