• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Zimbabwe lakanusha kufanya uasi

    (GMT+08:00) 2017-11-15 17:38:51

    Saa saba usiku wa kuamkia leomilipuko imesikika mjini Harare, Zimbabwe. Baadaye jeshi la nchi hiyo lilitoa taarifa kwa njia ya televisheni, likikanusha kuwa limefanya uasi, na kusema rais Robert Mugabe yuko salama, na kuwataka raia wote wadumishe utulivu.

    Jeshi la Zimbabwe limetoa taarifa hiyo saa 11 leo alfajiri baada ya milipuko.

    "Tunataka kuwaambia raia wa Zimbabwe, kuwa rais Robert Mugabe ambaye pia ni kamanda mkuu wa jeshi na familia wake wako salama. Tunawalenga wahalifu walioko karibu naye ambao wameiletea Zimbabwe matatizo ya kisiasa na kiuchumi, na kuwaadhabu."

    Kwenye taarifa hiyo, mwakilishi wa jeshi ameihimiza serikali, bunge na vyama mbalimbali viendelee na kazi zao, na kuwataka raia kudumisha utulivu.

    "Tunawataka raia wa Zimbabwe watulie, na kuepuka kutoka nje kama hakuna haja. Lakini kwa wale wenye kazi na wenye mahitaji ya kutoka, mnaweza kuendelea."

    Taarifa hiyo imesema madhumuni ya hatua zilizochukuliwa na jeshi ni kuwaadhabu kisheria wahalifu kwenye chama kitawala, na kurejesha hali ya kawaida ya siasa nchini humo haraka iwezekanavyo.

    Tarehe 6 mwezi huu Rais Robert Mugabe alimfukuza kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa, halafu chama kitawala cha ZANU-PF kilitangaza kumfukuza uanachama. Bw. Mnangagwa aliyekuwa mshiriki wa vita ya ukombozi wa Zimbabwe anaungwa mkono na jeshi, na alichukuliwa kama mrithi wa Rais Mugabe.

    Juzi mkuu wa jeshi la Zimbabwe Jenerali Constantino Chiwenga alitoa taarifa akikihimiza Chama cha ZANU-PF kuwatendea a haki wanachama walioshiriki kwenye vita ya ukombozi wa Zimbabwe, na kuacha kuwafukuza uanaxchama, na kusema jeshi halitakaa kimya na litachukua hatua zipasazo ili kuzuia hila ya wale wapinzani wa mapinduzi ya kuteka chama cha ZANU-PF. Taarifa hiyo imechukuliwa kama jibu la upande wa jeshi kwa amri ya Mugabe ya kumfukuza kazi Bw. Mnangagwa.

    Hivi sasa hali ya Zimbabwe ni shwari, na raia wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako