• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya biashara ya kuchangia matumizi ya China yafikia yuan trilioni 4.5

    (GMT+08:00) 2017-11-15 19:14:17

    Msemaji wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Meng Wei leo hapa Beijing amesema, inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, thamani ya biashara ya kuchangia matumizi ya China itafika Yuan trilioni 4.5 sawa na dola za Kimarekani bilioni 720, na itadumisha ongezeko la kasi ya zaidi ya asilimia 40 kwa wastani katika miaka kadhaa ijayo.

    Bw. Meng Wei amesema, ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa kasi ya uchumi wa kuchangia matumizi ya vitu kama baiskeli na nyumba katika miaka ya hivi karibuni nchini China. Amesema katika sekta ya uchumi wa kuchangia matumizi nchini China, kumekuwa na makampuni kadhaa yenye uwakilishi na baadhi yao yanaongoza katika soko hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako