• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Biashara wa Afrika Mashariki wajadili uwekezaji wa kikanda

    (GMT+08:00) 2017-11-15 19:34:05

    Viongozi wa biashara wanaoshiriki kongamano la pili la maonesho ya biashara na ujasiriamali la Afrika Mashariki,jijini Dar es Salaam Tanzania wanatafuta mbinu za kukuza ujasiriamali na kuvutia uwekezaji zaidi wa ndani na nje katika kanda.

    Maafisa wa ngazi za juu zaidi ya 300 wa serikalini na sekta binafsi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,pamoja na viongozi wa biashara,na wawekezaji katika kanda na ughaibuni wanahudhuria kongamano hilo.

    Kongamano hilo lilianza tarehe 14 na linatarajiwa kukamilika tarehe 16 Novemba,na limeandaliwa kwa ushirikiano na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

    Baraza la Biashara Afrika Mashariki linasema kuwa jumla ya thamani ya uwekezaji EAC imeongezeka kwa asilimia 6.9 hadi US$254.1m mwaka 2016 kutoka US$237.8m mwaka 2015.

    Mwaka 2015 jumla ya thamani ya uwekezaji EAC iliongezeka kwa asilimia 14.5 kutoka US$ 207.7 milioni mwaka 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako