• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya mafuta yapanda Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-15 19:34:51

    Wakati taifa la Kenya likiendelea kushuhudia msukosuko uliosababishwa na msimu mrefu wa siasa na uchaguzi wa urais,tume ya Kudhibiti nishati nchini (ERC) imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta.

    Bei ya petroli imeongezeka zaidi kuanzia Novemba 15 hadi Desemba 14 mwaka huu.

    Notisi ya ERC iliyotumwa kwa vyombo vya habari mapema jumatano imeonyesha kuwa petrol imeongezeka kwa Sh1.03, dizeli Sh3.70 na mafuta ya taa kwa Sh5.05 kwa lita.

    ERC imesema nyongeza hiyo imetokana na kuongezeka kwa bei ya mali ghafi ya kuunda mafuta.

    Imeongeza kwamba mali ghafi hayo, yalianza kuwa ghali kati ya Septemba na Oktoba 2017.

    ERC imesema kuwa nyongeza hiyo pia imechangiwa na kushuka kwa thamani ya dola ya Marekani na shilingi ya Kenya kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako