• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya Ipsos inaonesha kuwa wakenya wa maeneo ya mashariki na kati wanaumia kiuchumi

    (GMT+08:00) 2017-11-15 19:35:26

    Ripoti ya utafiti wa shirika la Ipsos nchini Kenya unaonesha kuwa maeneo ya mashariki na kati ya Kenya yanaongoza kwa idadi ya watu wanaokumbwa na hali ngumu ya kimaisha.

    Utafiti huo ambao ulifanywa kati ya Oktoba 14 na 22 unaonyesha kuwa asilimia 72 ya wakenya wanakabiliwa na hali ngumu za kiuchumi.

    Aidha Ripoti hiyo inaonesha kuwa miaka mitatu iliyopita mapato ya wakenya hayajakuwa yakiongezeka.Ripoti inaonesha kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi umekuwa ukinufaisha watu wachache mno.

    Idadi kubwa zaidi ya wanaoteseka ilikuwa eneo la mashariki mwa Kenya (asilimia 84), ikifuatwa na eneo la kati (asilimia 75), pwani (asilimia 74), Nairobi (asilimia 74) na Nyanza (asilimia 73).

    Sababu kuu zilizotajwa kusababisha hali hii ni gharama ya maisha (asilimia 36), uongozi mbaya (asilimia 34) na masuala ya uchaguzi (asilimia 12).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako