• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanyarwanda wahamasishwa kuweka akiba

    (GMT+08:00) 2017-11-15 19:36:27

    Juhudi za kukuza utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa wanyarwanda zimepigwa jeki kutokana na mpango wa kuhimiza umma,haswa mashirika,kuweka akiba na kuwekeza.

    Mpango huo unalenga kujenga jukwaa kwa viongozi wa biashara kujadiliana kuhusu mambo yanayoathiri uchumi.

    Afisa wa Rwanda Events ,ambao ndio waandaaji wa shughuli hiyo,Gaelle Kiyigi amesema wanataka kuwa na jukwaa ambalo litawawezesha wadau kujadiliana kuhusu mambo mbalimbali yanayoathiri sekta hiyo.

    Shughuli ya wiki hii ambayo itafanyika tarehe 16 jijini Kigali italenga kutafuta ufumbuzi wa kuziba pengo la kitaifa la uwekaji akiba.

    Mwezi uliopita serikali iliweka malengo ya kuongeza viwango vya kitaifa vya uwekaji akiba hadi asilimia 20 ya pato la taifa kufikia mwaka 2020 kutoka asilimia 10.6 ya sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako