• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege za za Russia zashambulia kundi la IS nchini Syria

    (GMT+08:00) 2017-11-16 09:25:18

    Wizara ya ulinzi ya Russia imesema ndege sita za Russia aina ya Tu-22M3 ziliruka kutoka Russia na kushambulia vituo vya kundi la Islamic State karibu na mji wa Albu Kamal katika jimbo la Deir al-Zour nchini Syria. Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inasema ndege hizo zilizopita katika anga ya Iran na Iraq ziliharibu ngome, magari na kuwaangamiza wapiganaji wa kundi la IS. Jana wizara hiyo ilitoa taarifa ikiushutumu muungano unaoongozwa na Marekani kwa kuzuia operesheni za jeshi la anga la Russia karibu na mji wa Albu Kamal, ambayo ni moja ya ngome za mwisho za kundi la IS nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako