• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yasisitiza kilimo kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2017-11-16 10:00:57

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limetoa taarifa likisema kiwango cha utoaji wa hewa ya ukaa kwenye sekta ya kilimo kinakadiriwa kuongezeka, na kuharakisha zaidi mabadiliko ya hali ya hewa.

    Kwenye mkutano wa 23 wa nchi zinazosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, mkurugenzi mkuu wa FAO Bw Jose Graziano da Silva amesema mabadiliko ya hali ya hewa yanawaathiri mamilioni ya watu kwa kufanya wawe na matatizo ya usalama wa chakula, utapiamlo pamoja na umaskini.

    Ameongeza kuwa kilimo si kama tu ni sekta inayoathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa, na bali pia ni chanzo kikuu kinachosababisha tatizo hilo, na kwamba mbinu zilizopo za kurekebisha sekta ya mifugo zinatarajiwa kupunguza asilimia 20 hadi 30 ya utoaji wa hewa ya ukaa kwenye sekta hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako