• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za kiarabu zatoa wito kuimarisha ushirikiano wa shughuli za baharini na China

    (GMT+08:00) 2017-11-16 10:08:48

    Mwenyekiti wa Shirikisho la Bandari la nchi za kiarabu ASPF ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya bandari za Kuwait Sheikh Al-Nassaer Al-Sabah, ametoa wito kuimarisha ushirikiano na China katika usafiri wa baharini kati ya nchi za kiarabu.

    Sheikh Al-Sabah amesema hayo baada ya kuhudhuria mkutano wa 52 wa kamati ya ASPF na mkutano wa pili wa uchukuzi wa nchi za kiarabu uliofanyika huko Alexandria, Misri.

    Bw. Al-Sabah amesema mkutano huo umejadili jinsi sekta ya usafirishaji na bandari zinavyonufaika na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lililotolewa na China.

    Ameongeza kuwa washiriki wa mkutano huo wameonyesha matarajio ya kuongezeka kwa uuzaji wa bidhaa za nchi za kiarabu katika soko kubwa la China, huku wakiamua kuandaa kongamano nchini Kuwait kujiandaa kwa ziara ya shirikisho la bandari za nchi za kiarabu nchini China, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu pendekezo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako