• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Tanzania nchini China atarajia mkutano wa 7 wa baraza la FOCAC utasaidia mchakato wa viwanda wa Afrika

    (GMT+08:00) 2017-11-16 17:47:47

    Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki amesema anatarajia kuwa mkutano wa 7 wa viongozi wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utazisaidia nchi za Afrika kutatua masuala ya nishati na miundombinu, na kuharakisha kutimiza mchakato wa viwanda wa Afrika.

    Bw. Kairuki anasema:

    "Serikali ya China ilitangaza kutoa msaada wa dola za kimarekani bilioni 60 kwa Afrika katika mkutano wa 6 wa FOCAC uliofanyika nchini Afrika Kusini. Ndani ya miaka 3 ya kutekeleza makubaliano ya baraza lijalo, tutahitaji nusu ya msaada wa sasa kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati. Lengo hilo likitimizwa, nchi za Afrika zitavutia wawekezaji wengi wa viwanda na kuongeza ajira. Aidha, makampuni madogo na ya kati yaliyoanzishwa na vijana na wanawake wa Afrika yatatoa mchango mkubwa kwa kuwasaidia watu maskini na maendeleo ya Afrika kutokana na upatikanaji wa umeme"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako