• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia na Marekani zapingana kuhusu kuongeza muda wa Tume ya kuchunguza matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria

     

    (GMT+08:00) 2017-11-16 18:17:34
    Russia na Marekani zinapingana kuhusu kama tume huru ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria inatakiwa kuongezewa muda au la.

    Mwezi uliopita, Russia ilipiga kura ya veto mswada wa azimio lililopendekezwa na Marekani ambalo lingeongeza muda wa mwaka mmoja zaidi wa Tume ya Uchunguzi ya Pamoja (JIM) ya Shirika la Kuzuia Kuenea Silaha za Kemikali na Umoja wa Mataifa.

    Ripoti iliyotolewa na JIM siku mbili baada ya Russia kupiga kura ya veto mwezi uliopita ilisema kuwa serikali ya Syria na kundi la kigaidi la IS zinawajibika kwa matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako