• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaorodhesha barafu inayowaka kuwa aina mpya ya madini

    (GMT+08:00) 2017-11-16 18:17:59

    China imeidhinisha kuorodheshwa kwa barafu inayowaka kuwa aina mpya ya 173 ya madini, hatua itakayoongeza kasi ya matumizi ya vyanzo vya nishati safi.

    Mkuu wa idara ya hifadhi ya nishati iliyo chini ya Wizara ya Ardhi na Maliasili Ju Jianhua amesema, China imefanikiwa katika kutafiti na majaribio ya ushimbaji majini na nchi kavu. Amesema, katikati ya mwezi Oktoba Wizara hiyo iliwasilisha kwenye Baraza la Taifa la China, ombi la kujumuishwa kwa barafu inayowaka kwenye orodha ya aina za madini, ombi ambalo limekubaliwa tarehe 3 mwezi huu.

    Mara ya kwanza China iligundua barafu inayowaka chini ya Bahari ya Kusini ya China mwezi Juni mwaka 2007, na kupata madini kwa mara ya kwanza mwezi Novemba mwaka 2008 katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Qinghai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako