• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akutana na kiongozi wa ujumbe wa China wa mkutano wa UNFCCC

    (GMT+08:00) 2017-11-16 18:37:35

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana huko Bonn amekutana na kiongozi wa ujumbe wa China wa mkutano wa UNFCCC ambaye pia ni mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia mambo ya mabadiliko ya hali ya hewa Bw. Xie Zhenhua, ambapo pande mbili zimebadilishana maoni kuhusu ushirikiano kati ya China na Umoja wa Mataifa kuhusu suala la mabadiliko ya hali ya hewa, kuhimiza dunia kukabiliana na suala hilo na masuala mengine.

    Bw. Guterres amesema, katika miaka ya hivi karibuni, China imeonyesha nguvu yake ya uongozi katika maendeleo ya uchumi, mazingira, hali ya hewa na sekta nyingine, na ni mwenzi muhimu wa ushirikiano wa Umoja wa Mataifa. Katika siku za mbele, Umoja wa Mataifa unapenda kuendelea kupanua ushirikiano na China, kuhimiza utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya mabadiliko ya hali ya hewa ya Paris, na kuhimiza dunia nzima kutimiza maendeleo endelevu.

    Bw. Xie Zhenhua amesema, ni lazima kuzingatia hali halisi ya mabadiliko ya hali ya hewa na suala la maendeleo wakati wa mchakato wa kuhimiza maendeleo endelevu. China inatumai Umoja wa Mataifa utahimiza nchi mbalimbali kutambua uratibu wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, kuhimiza dunia nzima kutimiza maendeleo endelevu na kutekeleza makubaliano ya Paris.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako