• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Dawa ghushi zagunduliwa tena Uganda

    (GMT+08:00) 2017-11-16 19:10:54

    Takriban mikebe elfu 10 ya dawa ghushi na dawa zilizoharibika zinaingizwa nchini Uganda na wafanyibiashara kinyume na sheria ya nchi hiyo.

    Halmashauri ya kitaifa ya dawa za matibabu nchini Uganda imetangaza kufanya awamu ya tatu ya oparesheni ya kuwatia mbaroni wauzaji wa dawa feki.

    Msemaji wa halmashauri hiyo Frederick Ssekyana amesema dawa aina ya Sutent na Avastin zimepatikana katika baadhi ya maduka nchini Uganda mwaka huu.

    WAhudumu wa afya nchini Uganda wanafanya oparesheni kote nchini humo kuchunguza dawa hizo .

    Wateja nchini Uganda wamekuwa wakiuziwa dawa hizo kwa shilingi milioni 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako