• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Mahindi ya nje marufuku kuingia Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-16 19:11:15

    Serikali imepiga marufuku uagizaji mahindi kutoka nchi jirani licha ya nakisi ya magunia milioni nane inayokumba nchi hii .

    Kulingana na katibu katika wizara ya kilimo Richard Lesiyampe serikali itawapa motisha wakulima kupitia bora kuuza mahindi yao kwa halmashauri ya kitaifa na nafaka na mazao NCPB ili kuondoa upungufu ambao umetokana na mavuno duni.

    Lesiyampe amesema kwa miaka mingi nchi hii imekuwa ikikosa kutimiza mahitaji yake ya mahindi na kulazimika kuagiza mahindi kutoka nchi jirani za Uganda na Tanzania Katibu huyo amekariri nia ya serikali kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa mahindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako