• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Wizara ya maji yaendeleza juhudi za kumaliza Uhaba wa maji Nairobi

    (GMT+08:00) 2017-11-16 19:12:09

    Waziri wa Maji nchini Kenya Eugene Wamalwa, ameahidi wakulima na wakenya kwa jumla kumaliza miradi inayotekelezwa na serikali katika juhudi za kumaliza upungufu wa maji wa lita milioni-250 jijini Nairobi.

    Mradi huo wa "Northern Water Tunnel" kutoka Murang'a, unatarajiwa kuongeza kiwango cha maji jijini Nairobi kwa lita millioni 140.

    Wamalwa amesema miradi sambamba ya kuhakikisha miji ya Mombasa, Kisumu na Nakuru inajitosheleza kwa maji.

    Kisumu itakuwa mji wa kwanza kujitosheleza kwa maji baada ya kukamilishwa kwa mradi wa maji wa Kisumu.

    Wakati huo huo, huduma za maji mjini Mombasa zitaboreshwa na kukamilishwa kwa bwawa la maji la Mwache na pia bomba la maji la Mzima Springs 2. Mji wa Nakuru utajitosheleza kwa maji baada ya kukamilika kwa bwawa la maji la Itare.

    Mpango wa kuboresha huduma za maji katika miji hiyo muhimu zaidi nchini, ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuongeza mara tatu uwezo wa kuhifadhi maji katika taifa hili, na pia kuongeza idadi ya wakenya walio na huduma bora za maji kutoka asilimia 60 kwa sasa hadi asilimia 80 itimiapo mwaka 2020

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako