• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Vijana washauriwa kujikita kwenye ujasiriamali

    (GMT+08:00) 2017-11-16 19:12:30

    Vijana nchini Rwanda wameshauriwa kujikita zaidi kwenye ujasiriamali ili kubuni fursa za ajira na kuchangia kwenye maendeleo ya uchumi.

    Meneja wa mradi wa maendeleo ya vijana William Furaha amebainisha kwamba ubunifu wa biashara na masuala ya uchumi ndio suluhisho la kudumu la kukabiliana na ukosefu wa ajira.

    Katika kongamano la kila mwaka la ubunifu wa biashara la vijana kilimo na sekta ya teknolojia ya kisasa ict zimetajwa kuwa kitega uchumi kikuu cha siku za sasa na baadae miongoni mwa vijana.

    Warsha hii iliyofanyika Kigali imewatuza vijana tofauti walioanzisha miradi mikuu ya maendeleo na faida kwa jamii mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako