• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya Nafasi za Ajira kwa wanafunzi wa Afrika wanaosoma China

    (GMT+08:00) 2017-11-16 19:18:55

    Takribani wanafunzi 400 kutoka Afrika wanaosoma vyuo vikuu vya China wamejitokeza kwenye maonyesho ya nafasi za ajira kwenye makampuni ya China yanayofanya kazi zake katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

    Katika maonyesho hayo makampuni 66 ya China yenye nafasi zaidi ya mia tano za ajira, yakiwemo yaliwekeza katika biashara ya nishati, mambo ya mawasiliano, teknolojia pamoja na makampuni yenye kandarasi za serikali au taasisi binafsi barani Afrika, yametumia fursa hiyo kuwaeleza wanafunzi taratibu pamoja na vigezo vinavyostahili ili kupata ajira katika kampuni husika.

    Ili kufahamu matarajio yao, Idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa imezungumza na baadhi ya wanafunzi wa vyuo tofauti waliojitokeza kwenye maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Biashara na Uchumi wa kimataifa cha mjini Beijing.

    Mtanzania Deusdedit Oygen ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili ya Mifumo ya Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Beijing na Aminata Bangura kutoka Liberia anayesomea shahada ya uzamili ya Utalii, walikuwa na haya ya kusema.

    Deusdedit "Ni furaha kuweza kupata nafasi ya kuona makampuni mbalimbali ya kichina, kuona mahitaji na vigezo, na kuona ni namna gani kama sisi watanzania tunaweza kushiriki, walioshiriki naanza kwa kuwapongeza, na wale ambao hawajaweza kuhudhuria, natoa wito kwamba kwa sababu maonesho hayo mwanzo,wajitokeze fursa zingine kama hizo zitakapojitokeza kwa ajili ya nchi zao na manufaa binafsi."

    Aminata "nilipopata taarifa za maonyesho haya nilifurahi sana, kwa sababu natarajia kupata kampuni ambayo itanisaidia kufanya mazeozi ya taaluma yangu ambalo ilikuwa ni vigumu kwangu kupata, na jambo la muhimu zaidi ni mahusiano yenye nguvu baina ya Afrika na China, zaidi nimegundua kuwa kuna kampuni inayoitwa BUCG hapa na inamiliki Hotel kule nyumbani Sierra Leone, na kwa kuwa taaluma yangu inalenga masuala hayo, kwa kuwa wanafanya vizuri hapana shaka kuwa sitakuwa na tabu tena."

    Kuhusu uhusiano wa makampuni ya China na nchi za Afrika, pamoja na mchango wake katika kusaidia jitihada za serikali husika za kuleta maendeleo ya kiuchumi, baadhi ya wanafunzi hao pia, kila mmoja ametaja baadhi ya viashiria vya mchango mkubwa uliotolewa na makampuni ya China wakiwemo, Brenda Jemutai kutoka Kenya ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Biashara na Uchumi wa KImataifa cha Beijing, na Emmanuel Maburk wa Sudan Kusini ambaye anasomea shahada ya Uzamili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Shandong.

    Brenda "Kampuni za China nyingi zimefanya mambo mazuri sana kule kwetu Kenya, kama vile kujenga barabara, kwa ujumla kutujengea miundombinu yote, ni nzuri sana ikilinganishwa na makampuni mengine hasa ya nyumbani, ambapo tukilinganisha, China wako mbele zaidi, hivyo itakuwa vizuri zaidi endapo tutapata maarifa hayo kupitia ajira."

    Emmanuel "hakika tukio hili ni muhimu sana, kwa kuwa kuna mahusiano makubwa sana baina ya China na Afrika kwa ujumla, lakini kwa nchi yangu ya Sudan Kusini, China imefanya na inaendelea kufanya mengi, na kwa upande wa maendeleo ya miundo mbinu, China imefanya makubwa, mfano mzuri uwepo wangu mimi ninasomeshwa na kampuni ya kichina iitwayo MuvCom na hii inatokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya China na Serikali yangu."

    Licha ya kuelezwa fursa zilizopo za ajira pamoja na taratibu ili kunufaika nazo, wanafunzi hao wameagizwa kukabidhi nyaraka za wasifu wao ili kukidhi matakwa ya ajira husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako