• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashambulizi ya anga yalenga ngome muhimu ya kundi la IS mashariki mwa Syria

    (GMT+08:00) 2017-11-17 09:30:53

    Mashambulizi ya ndege dhidi ya shabaha za kundi la IS yamefanyika mashariki mwa Syria katika mji wa al-Bukamal, ambayo ni ngome ya mwisho ya kundi la IS nchini Syria.

    Shirika la habari la Syria SANA limesema jeshi la anga la Syria limefanya mashambulizi makali kwenye njia za ugavi za kundi la IS kwenye maeneo karibu na mji wa al-Bukamal, kuwaua wapiganaji sita na kuteketeza silaha zao.

    Mwanzoni mwa mwaka huu jeshi la Syria lilitangaza kuukomboa mji wa al-Bukamal baada ya operesheni kubwa, lakini kundi la IS lilifanya shambulizi kubwa na kutwaa tena udhibiti wa mji huo.

    Mji wa al-Bukamal ni muhimu kimkakati kwa kundi la IS, kutokana na kuwa upo kwenye mpaka na maeneo ya Iraq yanayodhibitiwa na kundi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako