• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yaanza kutunga mswada wa sheria ya haki kwa watoto

    (GMT+08:00) 2017-11-17 09:40:59

    Serikali ya Somalia na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF wameanza kutunga mswada wa sheria ya haki kwa watoto, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha haki za watoto nchini Somalia.

    Baada ya kupitishwa, sheria hiyo itaweka msingi wa kuhimiza na kulinda haki za watoto wote, kufuatia kupitishwa kwa mkataba wa haki za watoto mwezi Oktoba mwaka 2015.

    Waziri wa wanawake na haki za binadamu Bibi Deqa Yusuf, na mkurugenzi wa UNICEF katika eneo la mashariki na kusini mwa Afrika Bibi Leila Pakkala wameshiriki kwenye utungaji wa mswada huo mjini Mogadishu, wakisema hatua hiyo inaonyesha imani kubwa ya kuwapatia watoto wa Somalia maisha bora.

    Bibi Yusuf amesema watoto wa Somalia wanakabiliwa na mapambano, ukame na changamoto nyingine. Kwa sasa inatakiwa kuimarisha mfumo wa sheria ili kuhakikisha wanapata haki ya maendeleo, elimu na ulinzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako