• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yasema gaidi wa Libya anahusika na shambulizi dhidi ya polisi

    (GMT+08:00) 2017-11-17 09:49:20

    Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imetoa taarifa ikisema, gaidi wa Libya aliyekamatwa alihusika na shambulizi dhidi ya polisi lililotokea hivi karibuni katika eneo la jangwa pembezoni mwa mkoa wa Giza.

    Taarifa imesema mpiganaji huyo wa Libya ni mtu pekee aliyebaki katika operesheni za usalama baada ya mashambulizi makali ya siku mbili ambayo yalianza Oktoba 20 na kusababisha vifo vya polisi 16 na wengine 13 kujeruhiwa, na mmoja aliyetekwa nyara aliokolewa baadaye na vikosi.

    Baada ya hapo kikosi cha usalama kilifanya shambulizi kwenye eneo la milima karibu na jangwa la magharibi na kuwaangamiza wapiganaji 15 na hatimaye kumkamata gaidi wa Libya aliyekimbia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako