• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya Umoja wa Mataifa yataka kupewa mamlaka mpya nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-11-17 09:49:42

    Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS imesema, ina matumaini ya kupata idhini mpya ya mamlaka yake itakayoisha katikati ya mwezi wa Desemba.

    Mkuu wa UNMISS Bw. David Shearer amesema, timu ya ukaguzi ya umoja wa mataifa inatarajiwa kwenda Sudan Kusini kusaidia kufanya mazungumzo na serikali na makundi mbalimbali kabla ya kutoa taarifa kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

    Timu hiyo pia itatumia siku mbili huko Addis Ababa ambako itakutana na makundi mengine ya nchi hiyo yakiwemo makundi ya upinzani.

    Pia ameeleza kuwa matokeo ya ziara ya timu hiyo yatasaidia kufikiwa kwa uamuzi wa baraza la usalama kati ya sasa na mwaka kesho katika kuidhinisha tena mamlaka ya UNMISS itakayoisha Desemba 15 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako