Akitoa sababu za pendekezo hilo Rais wa WADA Craig Reedie, amesema taifa hilo limekuwa likifanya udanganyifu katika vipimo vya wachezaji wake na limekaidi kuwapeleka wachezaji hao nje kwa ajili ya vipimo.
Ni mara ya pili WADA kupendekeza hivyo, baada ya kufanya hivyo pia mwaka jana wakati wa Olimpiki nchini Brazili licha ya kuwa pendekezo hilo lilitupiliwa mbali na Kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC.
IOC wanafanya mkutano mkuu Disemba 5, matarajio ikiwa ni kwamba huenda wakatolea majibu pendekezo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |