• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe na kamanda mkuu wa jeshi wakutana

    (GMT+08:00) 2017-11-17 10:08:56

    Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na kamanda mkuu wa jeshi la ulinzi Jenerali Constantine Chiwenga, na mjumbe maalumu wa rais wa Afrika Kusini wamkutana na kufanya mazungumzo mjini Harare. Gazeti la The Herald la Zimbabwe limeonyesha picha za viongozi hao wakikutana.

    Serikali ya Zimbabwe haijatangaza taarifa yoyote kuhusu mpango wa kisiasa katika siku za baadaye. Mkutano maalumu wa ngazi ya mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC uliofanyika jana mchana, pia haukutoa uamuzi kuhusu hali ya Zimbabwe, badala yake imependekeza kuandaa mkutano maalumu wa viongozi utakaoshirikisha viongozi wa nchi wanachama.

    Habari nyingine zimesema msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema sera ya kirafiki ya China kwa Zimbabwe haitabadilika licha ya hali ya hivi sasa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako