• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la 7 la mahakama na haki za binadamu kati ya China na Marekani lafanyika New York

    (GMT+08:00) 2017-11-17 10:15:10

    Kongamano la 7 la utekelezaji sheria na haki za binadamu kati ya China na Marekani, limefanyika huko New York, likihusisha wataalamu zaidi ya 20 wakiwemo wasomi, mahakimu na wanasheria kutoka pande mbili.

    Naibu mwenyekiti wa Shirika la mfuko wa maendeleo ya haki za binadamu ya China Bw. Huang Jin amesema mashirika yasiyo ya kiserikali ya nchi hizo mbili yakiimarisha dhana ya kuheshimiana, kujadiliana na kubadilishana maoni juu ya masuala ya haki za binadamu, kutakuwa na maana kubwa katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani.

    Kiongozi wa Kamati ya taifa ya uhusiano kati ya Marekani na China ya Marekani Bw. Stephen Orlins amesema uhusiano kati ya Marekani na China ni muhimu, na pia ni muhimu kudumisha mawasiliano juu ya haki za binadamu katika ngazi ya kiraia kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako